MMARAU Institutional Repository

TATHMINI LINGANISHI YA USAWIRI WA USHUJAA KATIKA TENDI ZA FUMO LIYONGO, MIKIDADI NA MAYASA NA SWIFA YA NGUVUMALI

Show simple item record

dc.contributor.author EVANS OMBENG’I NYACHOI
dc.date.accessioned 2026-01-22T10:05:37Z
dc.date.available 2026-01-22T10:05:37Z
dc.date.issued 2025
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/123456789/18769
dc.description.abstract Utafiti huu ni tathmini ya usawiri linganishi wa ushujaa katika tendi za Fumo Liyongo, Mikidadi na Mayasa na Swifa ya Nguvumali. Madhumuni ya utafiti huu ni kumtambulisha shujaa kwa vigezo vya ushujaa wa Kiafrika katika tendi teule za Kiswahili, kutathmini mchango linganishi wa mazingira katika kusawiri ushujaa katika tendi teule na kubainisha kiulinganifu matumizi ya mbinu za utunzi katika kusawiri ushujaa katika tendi teule. Uteuzi wa mada ya utafiti uliongozwa na kuwepo kwa pengo la kiusomi. Hata ingawa tafiti nyingi zimefanywa kuhusiana na swala la ushujaa, mtafiti hajaweza kutagusana na utafiti uliochunguza ulinganishi wa ushujaa katika tendi teule za Utendi wa Fumo Liyongo, Utendi wa Mikidadi na Mayasa na Utendi wa Swifa ya Nguvumali. Utafiti huu uliongozwa na nadharia tatu. Nadharia ya kwanza ni Mithiolojia iliyoasisiwa na Raglan (1936) na Rank (1909) na kuendelezwa na Okpewho (1979) na Mulokozi (2002). Nadharia ya Mithiolojia imeorodhesha sifa bainifu za shujaa wa Kiafrika ambazo shujaa wa Kiafrika anafaa kuwa nazo katika tendi. Nadharia ya pili ni Ujumi Mweusi ya Zirimu (1971). Nadharia hii inapendekeza fasihi ya Kiafrika ihusishe Uafrika na mazingira ya Kiafrika katika kusawiri ushujaa. Nadharia hii inalenga kuonyesha hali ya kujivunia Uafrika. Nadharia ya tatu ni Umaumbo ya Shyklovsky ( 1904) na kuendelezwa na Roman ( 1919). Nadharia ya Umaumbo inashikilia kuwa kazi za fasihi ziweze kuandikwa kwa sifa bainifu za umbo maalumu na zitumie mbinu mahususi za utunzi katika kufikisha ujumbe wa kifasihi. Utafiti huu ulikuwa wa maktabani. Maktaba mbalimbali yakiwemo ya intaneti yalitumika. Kundi lengwa la utafiti huu, lilikuwa tendi za Kiswahili, ambapo kimaksudi mtafiti aliteua tendi tatu ambazo ni Utendi wa Fumo Liyongo, (Kijumwa, 1913) Utendi wa Mikidadi na Mayasa, (Bashir 1972), na Utendi wa Swifa ya Nguvumali, (Ismaili 1968). Data imeandikwa kwenye nakala ngumu na pia kwa tarakilishi. Data ilikusanywa kwa njia ya uchanganuzi wa yaliyomo kwa kuzisoma tendi zenyewe na kazi mbalimbali zilizohusu suala la ushujaa. Uchanganuzi wa data ulikuwa kwa njia ya maelezo ambapo data ilieandikwa, ikachujwa na kufafanuliwa. Matokeo ya utafiti yamewasilishwa kwa njia ya maandishi. Utafiti huu umemtambulisha shujaa kwa vigezo vya shujaa wa Kiafrika katika tendi teule, na uligundua kuwa, si kila shujaa wa tendi teule za Kiswahili uafiki vigezo vya kumtambulisha shujaa wa Kiafrika. Mtafiti ametathmini mchango linganifu wa mazingira, na kuamua kuwa mazingira yana mchango mkubwa katika kumjenga shujaa katika tendi teule za Kiswahili. Kiulinganifu, utafiti uligundua kuwa, mbinu za utunzi zina nafasi kubwa katika kusawiri ushujaa. Mbinu nyingi zilitumika katika tendi zote ila tu mbinu za Ndoto na Ngomezi, ambazo zilitumika katika baadhi ya tendi. Matokeo ya utafiti huu yanatarajiwa kuwa ya muhimu kwa jamii ya wasomi katika urejeleaji wa dhana ya ushujaa na kuzua mtazamo mpya wa usawiri wa ushujaa kwa kulinganisha ushujaa katika tendi teule. Utafiti huu ni daraja kwa watafiti wa baadaye na ni nyongeza kwa tafiti ambazo zimefanywa kuhusiana na suala la ushujaa katika tendi za Kiswahili. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.title TATHMINI LINGANISHI YA USAWIRI WA USHUJAA KATIKA TENDI ZA FUMO LIYONGO, MIKIDADI NA MAYASA NA SWIFA YA NGUVUMALI en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account