MMARAU Institutional Repository

MUUNDO NA RUWAZA YA VIVUMISHI KATIKA TUNGO ZA KIIMENTI

Show simple item record

dc.contributor.author KENNETH KINYUA THURANIRA
dc.date.accessioned 2024-06-11T08:54:28Z
dc.date.available 2024-06-11T08:54:28Z
dc.date.issued 2023
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/123456789/15676
dc.description.abstract Utafiti huu ulishughulikia muundo na ruwaza ya kivumishi cha lahaja ya Kiimenti kinapotumika katika tungo za Kiimenti. Kiimenti ni lahaja mojawapo ya lugha ya Kimeru inayozungumzwa katika kaunti za Meru na Tharaka Nithi. Lahaja hii haijafanyiwa utafiti mwingi. Kwa hivyo, utafiti huu ni jitihada za kuongezea maarifa katika lahaja hii. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kubainisha aina za vivumishi katika lahaja ya Kiimenti; kuchunguza miundo ya vivumishi vya Kiimenti na jinsi usarufi unavyowakilishwa katika maumbo ya vivumishi; kupambanua ruwaza za usarufi katika vivumishi vya Kiimenti na kutathmini sheria za mpangilio wa vivumishi katika tungo za Kiimenti. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Sarufi Geuza Umbo Zalishi (Chomsky, 1957; 1965) na Nadharia ya Fonolojia Zalishi Asilia (Hooper, 1976). Nadharia ya Sarufi Geuza Umbo Zalishi ilisaidia kuchanganua maumbo ya vivumishi kimofemiki huku miundo ya nje na ndani ya vivumishi husika ikichunguzwa. Vivumishi vya Kiimenti hupitia michakato mingi ya kifonolojia vinapodhihirisha muundo wa nje kutoka muundo wa ndani. Nadharia ya Fonolojia Zalishi Asilia ilitumika kuchunguza michakato hiyo na sheria zinazohusika. Uchunguzi wa nyanjani na maktabani ulifanyika. Nyanjani, utafiti ulifanywa katika wadi ya Abothũgũchi ya Magharibi katika kaunti ndogo ya Meru ya Kati. Mbinu ya sampuli makusudi ilitumiwa kuteua eneo la utafiti na wasailiwa walioshirikishwa katika utafiti huu. Walengwa wa utafiti huu walikuwa wazungumzaji wazawa wa lahaja ya Kiimenti ili kuhakikisha uthabiti wa data. Mtafiti alihudhuria mikutano ya machifu, kanisa na ya wazazi shuleni ili kukusanya data ya vivumishi ambayo ilichanganuliwa. Mbinu za utafiti zilizotumiwa ni kurekodi mazungumzo ya wasailiwa katika mikutano hii kwa kutumia kalamu na karatasi pamoja na kinasa sauti cha rununu. Aidha, tasnifu, makala mahsusi na vitabu hasa vya hadithi katika lahaja ya Kiimenti na vingine vilivyohusu mada ya utafiti huu vilisomwa katika maktaba za vyuo vikuu vya Kenyatta, Nairobi, Moi, Egerton na Chuka. Kazi zaidi zilisomwa katika maktaba ya Wizara ya Elimu iliyoko jijini Nairobi ambapo tasnifu nyingi za vyuo vikuu mbalimbali zimehifadhiwa. Data ya vivumishi vya Kiimenti iliyopatikana ilichanganuliwa kwa kupanga aina mbalimbali za vivumishi katika majedwali na kuondoa uradidi uliojitokeza. Kisha vivumishi husika vilifanyiwa unukuzi wa kifonetiki na kutafsiriwa. Aidha, vilichanganuliwa ili kuamua utendakazi wa kisarufi ulioainishwa. Hatua nyingine ilihusu kupangilia sentensi zenye mpangilio sawa wa vivumishi pamoja na kuzifanyia unukuzi wa kifonetiki. Kisha zilitafsiriwa na sheria kuandikwa zilizodhibiti kila ruwaza ya vivumishi katika sentensi. Utafiti ulibainisha kuwa kivumishi cha Kiimenti huwasilisha muundo mahsusi wenye mofimu zinazotekeleza kazi za kisarufi. Inatarajiwa kwamba utafiti huu utakuwa mchango mkubwa wa kiisimu kwa kuwasaidia wanafunzi, walimu na watafiti wengine wakichunguza lugha za kiasili. Pia, utafiti utasaidia katika uhifadhi wa lahaja ya Kiimenti kwa vizazi vijavyo. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.title MUUNDO NA RUWAZA YA VIVUMISHI KATIKA TUNGO ZA KIIMENTI en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account