MMARAU Institutional Repository

Ufumbaji Katika Riwaya Za Katama Mkangi

Show simple item record

dc.contributor.author Ayiera, Elijah Arasa
dc.date.accessioned 2017-12-11T10:15:01Z
dc.date.available 2017-12-11T10:15:01Z
dc.date.issued 2017
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/123456789/6398
dc.description.abstract Utafiti huu umechunguza ufumbaji katika riwaya mbili za Katama Mkangi: Mafuta na Walenisi. Utafiti huu umelenga: Kwanza, kubainisha aina mbalimbali za ubunifu wa ufumbaji uliojitokeza katika riwaya ya Mafuta na Walenisi. Pili, kudhihirisha jinsi ufumbaji ulivyotumiwa na mwandishi kama kichocheo cha zinduko katika riwaya ya Mafuta na Walenisi. Tatu, kudhihirisha namna ufumbaji umeendeleza au kukwamiza usawiri wa wahusika wa mtunzi. Nne, kutathimini jinsi mazingira ya mwandishi yalivyochangia matumizi ya mafumbo katika riwaya ya Mafuta na Walenisi. Utafiti huu umebainisha kuwa, wakati ambapo Mkangi alikuwa akiandika riwaya hizi, uhuru wa kuikosoa serikali iliyokuwa mamlakani haukuwepo na kwa hivyo, alilazimika kutumia ufumbaji kuwasilisha ujumbe wake ili kuhepa rungu ya serikali. Pili, alikosomea na waandishi wengine, walimwathiri katika matumizi ya mbinu ya ufumbaji katika uandishi wake. Tatu, kutokana na kazi hii, ni dhahiri kuwa Mkangi alitumia mbinu ya ufumbaji kumzindua msomaji kuhusu athari za utabaka, ubepari, unafiki wa viongozi, sheria na nafasi yake katika jamii, umuhimu wa utu na usawa, umuhimu wa mapinduzi katika ujenzi wa jamii mpya, elimu na utafiti, mchango wa vijana katika ujenzi wa taifa miongoni mwa mengine. Aidha, imebainika kuwa Mkangi alitumia taswira, jazanda na istiari katika kufumba ujumbe wake. Hali kadhalika, imedhihirika kuwa ufumbaji ulimsaidia Mkangi katika usawiri wa wahusika wake kwa kuwapa majina ya majazi na lugha ya kimafumbo. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia Amali ambayo hupima umuhimu wa kitu kwa kuangalia matokeo ya matumizi ya hicho kitu. Nadharia hii hujishughulisha zaidi na matokeo na athari za hayo matokeo. Kwa hivyo, tumechunguza umuhimu wa ufumbaji kwa kuangalia matokeo na athari zake kwenye kazi za Mkangi. Utafiti huu ulifanyiwa maktabani na kwenye mtandao. Kwa jumla mafumbo yamechunguzwa na kuwekwa katika makundi kutegemea namna yalivyojengwa. Ukusanyaji wa data ulifanywa kupitia kwa mbinu ya uchanganuzi wa matini au yaliyomo. Data iliyokusanywa na kuchanganuliwa imewasilishwa kwa njia ya maelezo. Utafiti huu ni muhimu kwa njia mbalimbali. Kwanza, utakuwa kama mwongozo kwa waandishi wa baadaye kuandika kazi nzuri zaidi kimafumbo. Pili, utawasaidia wasomi kuelewa kazi hizi zilizoandikwa kimafumbo. Tatu, utafiti huu unachangia pia katika kuangalia riwaya za Kiswahili kitaaluma hasa kwa misingi ya ufumbaji kwa kutumia Nadharia Amali. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.title Ufumbaji Katika Riwaya Za Katama Mkangi en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Browse

My Account