MMARAU Institutional Repository

TATHMINI YA MATUMIZI YA LUGHA KATIKA UWASILISHAJI WA HABARI ZA MAZINGIRA KATIKA GAZETI LA TAIFA LEO LA KENYA

Show simple item record

dc.contributor.author NELLY NZULA KITONGA
dc.date.accessioned 2024-06-11T11:43:59Z
dc.date.available 2024-06-11T11:43:59Z
dc.date.issued 2023
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/123456789/15681
dc.description.abstract Utafiti huu unahusu tathmini ya matumizi ya lugha katika uwasilishaji wa habari za mazingira katika gazeti la Taifa Leo nchini Kenya. Gazeti la Taifa Leo huwasilisha habari kwa wasomaji kwa lugha ya Kiswahili. Lugha ya Kiswahili inatambuliwa na Katiba ya Kenya kama lugha ya taifa na pia lugha rasmi sambamba na lugha ya Kiingereza. Mazingira ni suala mtambuko na nyeti kitaifa na kimataifa. Mazingira yanaathiri maisha ya kila kiumbe kila siku kwa njia moja au nyingine. Inatarajiwa kwamba, kwa vile vyombo vya habari, Gazeti la Taifa Leo likiwemo, vimetwikwa jukumu la kuwapasha wanajamii yale yanayoendelea duniani kuhusiana na mazingira, vitafanya hivyo kwa namna ambayo itawawezesha watu kufahamu umuhimu wa mazingira na hivyo kuingiliana nayo kwa njia chanya. Hoja hii inatokana na imani kwamba mtu huthamini na kutunza kile anachofahamu thamani yake. Uchunguzi huu ulinuia kubainisha iwapo matumizi ya lugha katika kueleza habari za mazingira kwenye gazeti la Taifa Leo hufanikisha mawasiliano. Uchunguzi huu ulidhamiria kutimiza malengo yafuatayo: kuchanganua vipengele vya lugha vinavyoteuliwa na waandishi wa habari katika kuripoti habari za mazingira katika gazeti la Taifa Leo, kutathmini mtindo wa uwasilishaji wa habari za kimazingira na kubainisha ujumbe uliowasilishwa na waandishi wa habari katika gazeti la Taifa Leo. Nadharia zilizotumika katika utafiti huu ni Nadharia ya Uchanganuzi Usemi (NUU) iliyoasisiwa na Michel Foucault (1928) na baadaye ikaendelezwa na Norman Fairclough (1989) na Nadharia ya Umtindo (NU) ambayo iliasisiwa na Geoffrey Leech (1965-1966) na ikapaliliwa na Simpson (2004). Utafiti huu ulifanyika maktabani ambapo taarifa kuhusu habari za mazingira zilizochapishwa katika gazeti la Taifa Leo zilichanganuliwa. Magazeti ya Taifa Leo yaliyochapishwa kuanzia Januari 2021 hadi Machi 2022 yaliteuliwa kwa kudhamiria, hususan yale yaliyokuwa na habari kuhusu mazingira. Data ilikusanywa kwa kudondoa matumizi ya lugha, mtindo uliotumiwa katika uwasilishaji wa taarifa za mazingira kutoka magazeti ya Taifa Leo teule pamoja na aina na dhima za ujumbe uliojitokeza katika habari hizo. Utafiti huu ulichanganua matini 270 kutoka kwa magazeti ya Taifa Leo yaliyoteuliwa kimaksudi. Matini hizi ni zile ambazo zilifafanua taarifa zinazohusiana na mazingira. Data iliyokusanywa katika utafiti huu ilikuwa ya kithamano. Data ya kithamano ilikuwa zile habari zilizofafanua masuala ya mazingira katika gazeti la Taifa Leo. Data ya kithamano ilichanganuliwa kwa njia ya maelezo kwa kuzingatia mihimili ya nadharia teule. Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa maelezo, jedwali na takwimu. Inatarajiwa kwamba matokeo ya utafiti huu yatafaidi wanafunzi, watafiti, wanaharakati wa kimazingira, taaluma za Uchanganuzi Usemi, Umtindo na Pragmatiki, wanahabari, wachapishaji wa habari katika magazeti, na wasomaji wa habari hizo. Umuhimu wa Kiswahili kama wenzo wa mawasiliano pia umeangaziwa. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.title TATHMINI YA MATUMIZI YA LUGHA KATIKA UWASILISHAJI WA HABARI ZA MAZINGIRA KATIKA GAZETI LA TAIFA LEO LA KENYA en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Browse

My Account